Askofu
Dr. Charles Gadi akiongea na wanahahabari hawapo pichani kuhusu mkutano
wa maombi ya kitaifa wa kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.maombi hayo yatafanyika geita hivi
karibuni.
Na Sheila Simba,Maelezo
Askofu
Dkt Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais John
Magufuli,katika mchakato wake wa kuamishia serikali makao Makuu ya nchi
Mkoani Dodoma kwani ni uamuzi wa kijasiri na upaswa kuungwa mkono.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dare Es Salaam Askofu Gadi amesema kuwa
jitihada zinazofanywa na Rais magufuli ni kubwa kwani jitahada
zinaonekana wazi za kuimarisha mji wa Dodoma na ili uweze kutumika kama
makao makuu ya nchi.
‘’Serikali
inafanya kazi nzuri kinachotakiwa ni kumtia moyo Rias wetu ili jambo
ili lifanikiwe na kuhamisha serikali ili kutimiza mpango wa muda mrefu
wa kuhamisha serikali kutoka Dar es Salaam na kwenda Dodoma’’alifafanua
askofu Gadi
Aidha
amesema Serikali imejipanga na inaandaa mazingira mazuri kwa watumishi
wake watakao hamia huko kupata mahitaji yote muhimu wanayohitaji,na
kuongeza kuwa jambo hilo litaharakisha maendeleo katika mikoa jirani na
Dodoma.
Ameongeza
kuwa imekua ni kawaida ya baadhi ya watu kulalamika kila linapotokea
jambo bila kusikiliza na kufatilia jambo hilo kwa makini,amewaomba
watanzania wasiwe watu wakulalamika kulaumu na badala yake wawe watu
wakusiliza na kufata maelekezo.
Ameongezea
kuwa watafanya maombi ya kumuombea Rais John Magufuli na viongozi wa
serikali katika mji wa buselesele wilaya ya chato mkoani Geita agosti 25
mwaka huu,kuombea mvua,amani,upendo na mshikamano baina ya serikali na
wananchi wake.
No comments:
Post a Comment