Democratic Alliance kwa sasa kinashikilia baadhi ya miji mikubwa nchini humo
Chama
tawala nchini Afrika kusini ANC kimepoteza udhibiti katika jiji la
Johannesburg ambapo meya mpya wa jiji hilo Herman Mashamba anatoka chama
cha upinzani cha Democratic Alliance.
Chama cha ANC kipo madarakani tangu kipindi cha ubaguzi wa rangi nchini humo zaidi ya miaka 20.
Mashamba ameahidi kubadilisha utawala wa jiji.
ANC ilipoteza majimbo mengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita lakini bado ni chama kikubwa na kikongwe nchini humo.
BBC
No comments:
Post a Comment