Tuesday, March 8, 2016

WANAWAKE WAALIKWA KUJIONEA UCHIMBAJI BULYANHULU


Mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, akiwa na baadhi ya akina mama sehemu ya uchimbaji chini ya ardhi (underground mining), wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na wafanyakazi wa kike walipotembelea ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, jana Machi 8, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Bulyanhulu

KATIKA kuadhimisha kilele  cha siku ya Wanawake Duniani jana Machi 8, 2016, akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia,huko wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wao walitembelea na kuona shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi (Underground operations).

Akina mama hao kutka kada mbalimbali za vikundi vya wajasiriamali, wakulima, na viongozi wa dini, walifanya ziara ya kutembeela na kujionea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kiasi cha kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, walieleza kufurahishwa kwao na kusema hata wao wanaweza.

Pamoja na maeneo waliyoyatembelea, walijionea mashine za kuchironga miamba, pamoja na karakana (gereji) ya kutengeneza magar na mashine zinazotumika kwenye eneo hilo. Ziara hiyo iliwachukua takriban masaa matatu (3), na bila kuchoka walikamilisha  ziara hiyo na wote walikuwa katika hali nzur nay a furaha.

Katika tukio linguine, Mgodi huo ulimpatia kila mshiriki wa ziara hiyo, mche moja wa matunda ili wakapande kwenye maeneo wanayoishi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya mgodi kuhifadhi mazingira kwenye maeneo jirani na mgodi huo.

Siku ya wanawake Duniani, huadimishwa Machi 8 ya kila mwaka ili kuelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kutafuta majawabu yake.

Mama huyu ambaye ni sister wa kanisa Katoliki, alikuwa miongoni mwa wanawake waliotembelea mgodi huo chini ya ardhi

Ramadhani Chura, (kulia), mchimbaji wa madini chini ya ardhi, akiwapa maelezo akina mama hao umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi.

 Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimsaidia mama huyu akuvaa kibuyu cha gesi ya oxygen kabla ya kushuka chini ya ardhi.

No comments:

Post a Comment