MANCHESTER, ENGLAND
KOCHA wa Manchester United, Van Gaal, ameomba radhi kwa kitendo cha
kujiangusha juzi mbele ya mwamuzi wa akiba, Mike Dean, katika mchezo wa
Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Kocha huyo alijiangusha kwa makusudi huku akiwa na lengo la
kumuonesha mwamuzi jinsi wachezaji wa Arsenal wanavyojiangusha kwa
kumdanganya mwamuzi wa mchezo huo.
Kocha huyo alimwambia mwamuzi kwamba mshambuliaji wa Arsenal, Alexis
Sanchez, amekuwa mjanja hivyo mara kwa mara anajiangusha kwa ajili ya
kuomba ili waweze kutumia mipira ya adhabu.
Hata hivyo, Van Gaal amekiri kwamba alifanya makosa kuonesha mfano huo mbele ya mashabiki ambao walionekana kushangilia.
“Halikuwa jambo zuri kufanya mbele ya mwamuzi wa kati, mshika
kibendera na mwamuzi wa akiba, ninakubali kwamba nilifanya makosa na
natumia muda huu kuomba radhi kwa kitendo ambacho nilikifanya, japokuwa
mashabiki walionekana kufurahia.
“Nilifanya vile kutokana na hisia kali ambazo nilikuwa nazo kwa
wakati ule kutokana na mambo ambayo wachezaji wa Arsenal walikuwa
wanayafanya, lakini baada ya muda nikagundua kuwa si jambo zuri,”
alisema Van Gaal.
Credit: Mtanzania
No comments:
Post a Comment