Serikali imefunga kwa siku tatu Chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya rufani ya Tumbi Mkoani Pwani kutokana na hali mbaya ya chumba hicho ukiwamo ubovu wa majokofu na huduma isiyoridhisha.
Akizungumza
mara baada ya kufanya ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala amesema amechukua
uamuzi huo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa chumba
hicho.
Naibu
waziri amesema amekuta changamoto kadhaa katika chumba hicho ikiwemo
ubovu huo wa Mjaokofu hali inayosababisha maiti kulazwa sakafuni, na
kupelekea kuharibika na kutoa harufu kali.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Kigwangala amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa
Shirika la Elimu Kibaha kuandika barua ndani ya msaa 24 ya kujieleza
kwanini asifukuzwe kazi kutokana na kushindwa kutatua changamoto
zinazoikabili hosptali teule ya Tumbi.
Naibu
Waziri huyo amesema amebaini kuwa kuna tatizo la kiutawala hali
inayosababisha utoaji wa huduma za kimatibabu kuwa wa kusuasua ikwamo
kukosekana kwa maji,ubovu na uchakavu wa chumba cha upasuaji, ukosefu wa
dawa na chupa za kuhifadhia damu.
No comments:
Post a Comment