Wednesday, March 2, 2016

Serikali kuwachukulia hatua waharibifu wa Mazingira






Na PC  William-Mpwapwa

Idara ya usafi  na mazingira wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma hii leo imetoa taarifa ya hatua zilizochuliwa dhidi ya uharibifu wa mazingira kwa barua namba HW/MPW/M10/20/78 ya 29/02/2016.
Akitoa taarifa hiyo mkuu wa idara ya usafi  wa mazingira Bw.Emmanuel Saro, kuwa wilaya ya Mpwapwa ina kata 33 lakini baadhi ya kata kama Berege na Lufu angalau zimetekeleza sehemu ya adhabu kama sheria ndogo ya Halmashauri no 13 ya Mwaka 2002 inavyosema, mtuhumiwa anatakiwa kulipa faini ya shilingi laki tatu au kufungwa jela kwa muda wa miezi 6 hadi 12 au vyote kwa pamoja.

Pia ameendelea kutoa ufafanuzi  kuhusu kata zisizotekeleza wajibu wao na zenye uharibifu mkubwa wa mazingira kwa barua yenye no HW/MPW/M.10/20/86 ya 17/02/2016, kuwa uongozi husika unatakiwa kuainisha na kuorodhesha waharibifu wa mazingira wote, kuhakikisha wahalifu wote  wanafikishwa kwenye baraza la kata kwa hatua za kisheria, kuhakikisha wanapanda miti eneo lililo haribiwa na kuhakikisha kuwa hatua zote za utekelezaji na matokeo yanaifikia ofisi ya usafi na mazingira kabla ya siku 21, alieleza kata hizo ni Chunyu,Mima,Iwondo,Nghambi,Manghaliza,Luhundwa,Chitemo,Massa,Kimagai,Pwaga,Malolo,Wotta,Gulwe,Kingiti,Ipera,Berege,Mlunduzi pamoja na Rudi.

Sambamba na hayo ameeleza changamoto mbalimbali wanazozipata kutoka kwa uongozi wa ngazi za chini yani watendaji wa kata na vijiji kutokuwa na ushirikiano katika kutimiza adhma hiyo.

Hata hivyo WazoHuru imemtafuta kwa njia ya simu mtendaji wa kata na vijiji japo hakuweza kupatikana kuthibitisha jambo hili.

No comments:

Post a Comment