Baadhi ya vijana walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa sasa wameacha
Mlezi wa
kituo hicho cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu kushoto akiwa na
baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao
wanaishi kituoni hapo
Shadrack
John ambae anaishi kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa
Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za
kulevya
Na MatukiodaimaBlog.
KAMANDA
wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa
Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya
madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli
kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa
madawa ya kulevya mkoani hapa.
Bw
Asas ambae wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka
bayana mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya
madawa ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House
kilichopo Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao
ambao afya zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusana na
kuwapatia tiba.
Akizungumza
na mtandao wa matukiodaima leo Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi
wa NGOs ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings
(FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa madawa
ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza kufanya kazi
chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas .
Alisema
kuwa kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi
mmoja ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo
hicho pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji
wa dawa za kulevya ambao kwa sasa waliacha .
"
Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu na
Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika na
madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni kumuunga
mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya madawa ya
kulevya ......hivyo bado tunaomba wadau wengine kujitokeza
kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu "alisema Dr
Ngalla
Kuwa
lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya
kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga kuwafikia
vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo tafiti
zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya madawa ya
kulevya .
Msimamizi
wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa
kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya FADAS
ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho .
Alisema
kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni
hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo na
mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na
hivyo kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya
kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw Shadrack
John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja kupatiwa
huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri zaidi.
No comments:
Post a Comment