Trump anaongoza miongoni mwa wagombea wa Republican
Shirika
moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa
miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia.
Shirika
hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump
atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na
kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani.
Hata
hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye
kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha
Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema
"ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic".
Ushindi
wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata
Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya
kivita katika bahari ya South China Sea.
Kuyumba
kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na
kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo
yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa Bw Trump.
"Kufikia
sasa, Bw Trump ametoa maelezo machache sana kuhusu sera zake, na huwa
anabadilisha sana msimamo wake,” EIU wanasema kwenye ripoti yao ya
utathmini wa hatari zinazokabili dunia.
Utathmini huo huangazia pia athari za jambo fulani na uwezekano wa jambo hilo kutokea.
Al-Shabab
wamtumia Trump wakitafuta wafuasiUS: Maneno ya Trump ni hatari kwa
usalamaAdele:Trump hana idhini ya kutumia nyimbo kisiasa
EIU
hutumia kipimo cha moja hadi 25, na Bw Trump ana alama 12, sawa na
hatari ya "kuongezeka kwa ugaidi wa kijihadi kuathiri uchumi wa dunia”.
"Amekuwa
na msimamo mkali sana dhidi ya biashara huria, pamoja na Nafta, na
ameituhumu Uchina mara nyingi kuwa taifa linalofanyia mchezo sarafu,”
EIU inasema.
Shirika hilo limeonya kuwa matamshi yake makali dhidi ya Mexico na Uchina hasa yanaweza kusababisha vita vya kibiashara.
Bw Trump
amependekeza ua ujengwe kati ya Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji na
pia ametetea kuuawa kwa jamaa za magaidi. Aidha, amependekeza kuvamiwa
kwa Syria ili kuangamiza kundi la Islamic State.
EIU
wanasema pendekezo msimamo wake kuhusu mzozo Mashariki ya Kati pamoja na
pendekezo kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani vinaweza kutumiwa na
makundi ya itikadi kali za Kiislamu kuwatafuta wafuasi zaidi.
CREDIT:BBC
No comments:
Post a Comment