Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitia
umuhimu wa Chama cha Watoa Huduma za Mitandao (TISPA) kuongeza watoa
huduma hao ili kupunguza gharama za mitandao lakini kuongeza kasi ya
mtandao.
Mwenyekiti
wa Chama cha Watoa Huduma za Mitandao (TISPA) Vinay Choudary
akimhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa namna chama chake kilivyojipanga kuongeza watoa huduma za
mtandao wakubwa ili kupunguza gharama za mtandao na kuuwezesha kufanya
kazi kwa kasi.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikata utepe
ishara ya kufungua moja ya mtambo utakaowezesha kasi ya mtandao hapa
nchini.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekitaka Chama
cha Watoa Huduma za Mtandao nchini (TISPA), kuhakikisha watanzania
wananufaika na fursa za uwepo wa mkongo wa taifa.
Amesema
Serikali imejenga kilomita 7,560 za mkongo wa taifa nchi nzima ili
kuhakikisha huduma za mtandao zinakuwa kwa haraka na zinapatikana wakati
wote ili kuhuisha huduma na uchumi wa wananchi.
Akizungumza
mara baada ya kufungua moja ya mitambo ya kuongeza kasi ya mtandao
unaosimamiwa na TISPA, Prof. Mbarawa amesema huu ni wakati wa watanzania
kunufaika kwa kutumia mtandao wenye haraka na wa bei nafuu.
“Hakikisheni
mnaleta watoa huduma za mtandao wengi ili huduma hiyo ipatikane kila
mahali, kila wakati na kwa bei nafuu”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha,
Waziri Mbarawa amesema Serikali imetumia dola za kimarekani Milioni 12.2
kwa ajili ya kuboresha huduma za mtandao na kupeleka huduma kwa
wananchi hivyo watu watumie fursa hiyo kujiletea maendeleo.
“Tumieni
mtandao kupata elimu na kukuza uchumi, tuachane na matumizi yasiyo na
tija yanayotupotezea muda na kutufundisha vitu vinavyoweza kuathiri
maadili yetu kwa mtu mmoja na taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Amekemea
vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma kutumia mtandao kwa masuala
yasiyohusika na kazi wakati wa kazi na hivyo kupoteza muda hali
inayodhorotesha utendaji wa siku kwa siku.
Prof.
Mbarawa ameitaka TISPA katika kipindi cha mwaka mmoja kuhakikisha
inaleta kampuni kubwa za mtandao hapa nchini ili kuwa na maudhui ya
kimataifa, kuwa na mtandao wenye kasi, na kuwezesha huduma za mtandao
kuwa za bei nafuu.
No comments:
Post a Comment