MTU
mmoja mwenye umri wa miaka 80 amekutwa akiwa amefariki ndani ya choo
cha msikiti wa Ibadhi ulioko Bopwe karibu na Ofisi za Baraza la
Wawakilishi Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi ofisini Kwake , Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba Kamishina msaidizi Hassan Nassir Ali alisema aliyefikwa
na mauti hayo ni Hassan Ali Juma mkaazi wa Bopwe Wete .
Alisema
mzee huyo aliondoka nyumbane kwake machi 9 majira ya saa saba ,
kuelekea msikitini kwa ajili ya maandalizi ya swala ya adhuhuri , na
kuonekana machi 10 majira ya saa 12.45 jioni akiwa amefariki ndani ya
choo .
Inadaiwa
kuwa mzee huyo baada ya kufika msikitini aliingia chooni kisha
kufunga mlango kwa ndani ambapo alianguka akiwa katika harakati za kufua
fulana alilokuwa amevaa ili aoge.
“Tumebaini
kwamba mzee huyo alianguka katika harakati za kuvua fulana , ambapo
tumemkuta akiwa amefunikwa na fulana usoni huku akionekana kuumia zaidi
sehemu za kichwani ”alifahamisha .
Akizungumza
katika eneo la tukio Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jina wa jeshi la
Polisi Mkoa Issa Juma Suleiman aliwataka wananchi kutoa taarifa katika
jeshi la Polisi wanapopotelewa na jamaa zao ili wasaidiane kuwatafuta .
Alieleza
kwamba tangu mzee huyo alipopotea hakuna mtu aliyefika na kutoa taarifa
katika jeshi la Polisi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu .
Naye
mdogo wa marehemu Khamis Ali Juma (42) alisema kabla ya kufikwa na
mauti hayo kaka yake hakuwa na matatizo yoyote kiafya , na aliondoka
nyumbani kwa ajili ya kuwahi swala ya Adhuhuri katika mskiti wa Ibadhi .
No comments:
Post a Comment