Na PC William Mpwapwa.
Jeshi la
Polisi Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma hii leo limefanya utambulisho wa kamanda
mpya wa Polisi Wilayani humo ambapo Kamishna
Razaro Benedict Mambosasa, ndiye anachukua nafasi hiyo kuliongoza Jeshi la
Polisi.
Kamishna
huyo ambaye ametokea makao makuu ya polisi, amefurahishwa na askari wa wilaya
ya Mpwapwa kwa kuonyesha nyuso za furaha wakati wakiimba nyimbo ya maadili
ya jeshi la polisi.
Akikabidhi nafasi hiyo Kamishna David Misime, amesema kwamba mfumo wa utaratibu na sheria za mwongozo wa jeshi la polisi upo palepale hivyo hivyo jeshi hilo litarajie mabadiliko ya mfumo wa kiutawala, zaidi sana kuongeza uhusiano hasa kwa kile anacho kihitaji katika utawala wake kwa jinsia zote.
Aidha
ameeleza kuwa lengo kuu la jeshi la polisi Wilayani humo ni kutimiza malengo na
madhumuni ya jeshi hilo,pia kutoogopa malalamiko kutoka kwa watu wengine,
dhahiri ni kuwa na nidhamu na kuonyesha ushirikiano katika uongozi mpya ili
kurahisisha utendaji wa kazi.
"Mimi
ni kama mzazi na mlezi"ila endapo utakuwa katika nafasi yako ya
uwajibikaji, pia sipendi askari wachache wafanye kazi kwa faida ya askari wengi
hivyo ninawasihi askari wote wawajibike"Alisema
Kamishna Mambosasa
Nae mkuu wa polisi wilaya ya mpwapwa afande Francis Duma ameonyesha kuwa bega kwa bega katika hotuba ya viongozi hao na kuongezea juu ya umoja wa askari katika utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment