Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutoa lugha
chafu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayomkabili
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, Aprili 13, mwaka huu.
Hukumu
hiyo itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa
mashtaka unaowakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi
Mutalemwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Kibatara kuwasilisha
hoja zao za mwisho.
Uamuzi
huo ulitolewa jana na mahakama hiyo baada ya Kubenea na mashahidi wake
watatu, akiwamo mwandishi wa New Habari 2006, Shabani Matutu na Josephat
Isango wa Mwanahalisi kutoa ushahidi wao.
Akitoa
ushahidi wake, Matutu alidai kuwa Desemba 14, 2016 katika Kiwanda cha
Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa
wafanyakazi, hakusikia Kubenea akimuambia Makonda kuwa ni mjinga,
mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe kapewa.
Alidai
alimsikia mbunge huyo akimuuliza Makonda “kwa nini unafunga mkutano
bila ya kunipa nafasi ya kuongea wakati mgogoro nimeuanza mimi kuutatua,
mimi siyo kibaka nimekuja baada ya kuitwa na wananchi walionichagua kwa
kura 87,000”.
Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment