MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho
vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani
kwenda kazini.
Katika
hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki
katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lisonge mbele badala ya
kuwa watazamaji.
Makonda
aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya
Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo
vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia
mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
"Nawaomba
watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo
yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu
Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila
kitu akifanye yeye" alisema Makonda.
Makonda
alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu
hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu
ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.
No comments:
Post a Comment