Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam ambapo amesema
kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato
na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh.
trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850.
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendejana, Jinsia,
Watoto na Wazee Mpoki Ulusubisya.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa
waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo
ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba
mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari
wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo
waliyojiwekea.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Ufundi Tarishi Kibenga
amesema Wizara yake itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na
malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa
wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.
Katibu
Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Watoto na
Wazee akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha
walizopata mwezi huu ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo
yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha
Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam.
Baadhi ya
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari jana
jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya
vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari
mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo
zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850.(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Na Nyakongo Manyama –MAELEZO-Dar es salaam
Serikali
imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu
tofauti na zilizokuwa zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi
cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya
maendejana.
Takwimu
hizo zimetolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali
ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu.
Amesema
kuwa kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7
kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule
za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo
ya ada,chakula pamoja na ruzuku.
Katibu
Mkuu huyo ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es salaam imeongezewa shilingi
bilioni 2 ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika
mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo.
Aidha,
Dkt. Likwelile amesema kuwa ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni
na wakufunzi wao ,Wizara imetoa shilingi Bilioni 1.65 kwa ajili ya
mafunzo kwa vitendo.
Kati ya
fedha hizo wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio
masomoni wametengewa shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya
kufundishia, posho na nauli.
Ameongeza
kuwa fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7
zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Umma , ulipaji wa
deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko
ya hifadhi za Jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13.
Fedha kwa
ajili ya shughlui mbalimbali za maendejana zimetolewa kiasi cha
Shilingi Bilioni 166.2 ambapo chuo kipya cha Sayansi kilicho katika
hatua ya ujenzi cha Mlunganzi la kimepatiwa Shilingi Bilioni 18 na Kiasi
cha Shilingi Bilioni 13.6 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya
juu.
Mamlaka
ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi Bilioni 23.078, Mpango wa Maji
vijijini Bilioni l7.1, maendejana ya ujenzi wa barabara zimetolewa
shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini zimetengwa shilingi
bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa
shilingi bilioni 4.5, na Mahakama zimepatiwa shilingi bilioni 12.3.
Naye
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema
kuwa makusanyo yameongeza kutoka shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi
Disemba hadi kufikia trilioni 1.79 kwa mwezi Januari
No comments:
Post a Comment