Monday, February 15, 2016

Neno La Wakati Mwema TUKIMTEGEMEA MUNGU TUTASHIDA MAJARIBU


Na Mathias Canal

Kwa mujibu wa kalenda ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania leo ni siku ya Bwana ya Sita kabla ya Pasaka na ukisoma kwenye muongozo wa ibada ya kila jumapili yaani Liturugia Ukurasa wa 417 unaweza jifunza afa ya siku ambayo dhahiri inaonyesha namna ya kuyashinda majaribu kama ukimtegea Mungu lakini.

Neno Majaribu ni neno lenye ujumbe na tafsiri pana, tunaposema majaribu kwa maana ya kikristo na kiswahili fasaha ni jaribio ambalo linajitokeza lakini lina majibu mawili ama kulikabili au likukabili lenyewe.

Jumbe mbalimbali zinaelekeza kwa ufasaha kupitia maandiko ya Biblia Takatifu ukisoma maandiko ya Mwinjilisti Marko 1:12-13 inasema Mara Roho akamtoa aende Nyikani, Akawako huko jangwani siku Arobaini hali akijaribiwa na shetani naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walikuwa wakimhudumia.

Mwinjilisti Marko amejitahidi kuwajuza watu kuwa Yesu alijaribiwa kwa kiasi kikubwa lakini bado aliyashinda majaribu, kuyashinda kwake majaribu ikawa mtaji wa Wakristo kiimani na ndio mana leo wakristo tupo katika siku ya Sita ya Mfungo wa Kwaresma.

Hivi karibuni kwenye moja ya makala zangu nilizoandika nilijikita zaidi kuwakumbusha wakristo kwamba kuna kufunga na kushinda njaa.

Kufunga sio lazima iwe kula, unaweza ukafunga baadhi ya vyakula ama ukafunga kunywa maji lakini yawezekana ukafunga baadhi ya tabia, lakini ili mfungo wako ukamilike ni lazima uambatane na Maombi ya siku nzima na hatimaye siku zote Arobaini.

Lakini kama kuna mkristo ataacha kula siku nzima kwa maana ya kufunga lakini maombi akawa hayafanyi hakika atakuwa anashinda njaa na ni dhahiri kuwa namkumbusha ni bora akaendelea kula tu kuliko kupoteza muda.

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania Ambwene Mwansongwe amewahi kusikika na maneno mema kwenye moja ya nyimbo zake akisema acha tuteseke, ulimwengu ututese, watu watusimange na kutunenea mabaya lakini Hatutaogopa ujasiri wetu kwani tutaendelea kumfuata Yesu.

Nimeanza kuelezea majaribu huku nikiamini kwamba tukimtegemea Mungu tutashinda majaribu hayo lakini tuwe na mategemeo ya imani kwani Majaribu yanatuunganisha sisi wanadamu japo kuna wakati tunajisahau na kujikita kupambana katika vita ya kimwili kuliko Vita ya kiroho ama Imani (Maombi).

Mwimbaji Ambwene aliposema majaribu ni mtaji alijikita kuwajuza kuwa Msingi wa imani ni sala, lakini watu wanapaswa kukumbuka kuwa shetani hajali kwamba wewe ni mchungaji, Muombaji, mkeshaji kanisani, Mwinjilisti, Parishi Waker ama Askofu ila anamjaribu kila mtu na ndicho kipimo cha imani.

Hakika tukimtegemea Mungu tutayashinda Majaribu, kwani majaribu ni Mtaji na msingi wa Imani.

Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal
0756413465
Dodoma

No comments:

Post a Comment