Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ZEC akifutilia mbali matokeo ya uchaguzi
Marekani
imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya
uchaguzi wa rais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani
humo.
Katika
taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa ubalozi huo nchini Tanzania,
Marekani ilisema imeshtushwa na hatua hiyo na kutoa wito tume hiyo
iondoe tamko hilo.
Zec imeahidi kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.
Katika
kufutilia mbali matokeo ya urais wa Zanzibar, tume ya uchaguzi ya
Zanzibar-ZEC ilisema shughuli nzima ya upigaji kura visiwani iligubikwa
na kasoro nyingi.
Hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amesema baadhi ya
makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa
kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".
"Kumegundulika
kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa
baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la
wapiga kura wa kituo husika."
Amesema
hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura
hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura".
Taarifa ya ubalozi wa Marekani inasema kufutilia mbali matokeo hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi
Kadhalika,
amesema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako
amesema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika
kisiwa hicho walifukuzwa.
Hata
hivyo, taarifa ya ubalozi wa Marekani inasema kufutilia mbali matokeo
hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.
Aidha
Taarifa hiyo inasema kuwa hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar
inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi kutoka
ubalozi wa Marekani, jumuiya ya ulaya, jumuiya ya madola na jumui ya ya
maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kuwa uchaguzi huo ulikuwa
wa haki.BBC
No comments:
Post a Comment