
Baadhi ya
wasanii wa Bongo Movie na wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa
kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.
>

Mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo
la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM
ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za
kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua
kwa biashara anuai.
Alisema
Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya
maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji
maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa
mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge
zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.(P.T)

Kulia ni baadhi ya wasanii maharufu wa uigizaji wakishangilia wakati Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Mwisenge.

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Sirari wakifikisha ujumbe wao kwa Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipohutubia wananchi katika viwanja vya Tarafa Sirari.
No comments:
Post a Comment