Monday, August 17, 2015

MABASI YA MWENDO KASI SASA BARABARANI..

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSO1jUjwEeEyK3knzFu7UpIzMBtOGaaEvTq0yp9wfBZAWZwnDvD9tcbCm3krQA3dm4YkcMsEms8e0pAnu7Ey_DM5FPloZQygCJWb3f8p6UcKmp4lDiL-8wYKc0AEghISbXKwWsSBirbCw/s1600/DSC_0300.JPG

SERIKALI imewataka madereva walioanza kupata mafunzo ya kuendesha mabasi yatakay
 otumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kuzingatia mafunzo hayo ya kihistoria hapa nchini.
Mafunzo hayo yaliyoanza jana ni moja ya matayarisho ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito mwezi Oktoba mwaka huu.

Akifungua rasmi mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia aliwataka madereva hao kuyapokea kwa bidii na umakini mkubwa.

“Mafunzo haya yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa,” alisema wakati wa maadhimisho hayo katika eneo la Ubungo.
Waziri Ghasia aliieleza kwamba mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo yatahusu pia namna ya kuhudumia wateja.

“Madereva hawa watajengewa weledi na nidhamu katika kazi yao ambayo kwa sasa inalalamikiwa sana na wananchi wakilalamikiwa kwa utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiki alisema kuzinduliwa kwa mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira ya serikali kutatua kero ya usafiri na msongamano wa magari jijini humo kupitia mradi wa BRT.

“Mradi huu wa aina yake nchini na barani Afrika utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi,” alisema.

Mafunzo hayo kwa madereva wazalendo yanafanyika baada ya kushinda usaili ulio endeshwa na wataalamu kutoka chuo cha ufundi stadi na mafunzo (VETA).

Jumapili iliyopita kampuni ya watoa huduma wa ndani wa mradi huo, UDA-RT iliendesha semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na huduma za kipindi cha mpito za mradi huo.

Mradi huo wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara maalum kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kutoka Faya hadi Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi eneo la makutano ya Morocco.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1jMYNIPEVnGxAWhbD7AS-PK_FJjy1-woEANab4WdAeGgAcet6nfv6u_mY-V_j72gGUbwCIIjMk6u3VsGF_2lcKV8u-q2yZtkTOBeYGlHjW-M9JL3ekLmQqG9YWkXTHAwEdeWJM9XfDhk/s1600/DSC_0116.JPG

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1Nj8alyoDYs5PyXpApNteNsEodqkSB2kkOAxLiBijCBWW16knAzMhmksCcibUMSsRmJmtpeXgbLle4r0fEZehAq-dG9123ooLemS-cal9xg8IOBm_R1FLzBw4fJmJwdXFIv71fksuj2I/s1600/DSC_0278.JPG

No comments:

Post a Comment