Tatizo la kupata mawasiliano ya simu kwenye vituo vya usafiri vilivyojengwa chini ya ardhi nchini Afrika Kusini limekuwa ni tatizo sugu kwa muda mrefu.Kituo maarufu cha Gautrain ambacho kimekuwa kikitumiwa na wasafiri wengi wakiwemo wanafunzi,wafanyakazi na watalii kwa muda mrefu tangia kifunguliwe mwaka 2010 kimekuwa kikikabiliwa na tatizo la mtandao ambao ulisababisha wasafiri wanaokitumia kituo hicho kushindwa kuwasiliana kwa njia ya simu na barua pepe.
Kampuni
ya Vodacom imejitosa kumaliza tatizo hilo kwa wateja wake ambapo kwa
kushirikiana na Idara inayosimamia usafiri wa reli na barabara,uongozi
wa kituo cha Gautrain,makampuni ya Bombela na Strategic kwa pamoja
makampuni hayo yanafanya mchakato wa kumaliza tatizo la mawasiliano
katika kituo hicho.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Ukuzaji Teknolojia wa kampuni ya Vodacom Afrika ya
kusini Andries Delport anasema “Siku zote nilikuwa nakerwa na kukosekana
mtandao wa mawasiliano ya simu na internet kwenye vituo vya treni
vlivyopo ardhini hali ambayo imekuwa ikiwasababishia usambufu
abiria.Tunajivunia kuwa mtandao wetu mkubwa nchini Afrika ya Kusini
tumeamua kumaliza tatizo hili kwa wateja wetu”
Tatizo
hili litamalizika kutokana na vifaa bora vya mawasiliano vilivyofungwa
na Vodacom katika vituo vitatu vya treni za ardhini,vifaa hivyo vya
kisasa ambavyo ni pamoja na antenna za kurusha mawasiliano
zimeunganishwa na mkongo wa mawasiliano uliopo eneo la Rosebank na hatua
hii pia itawezesha upatikanaji wa huduma za internet kwa urahisi.
“Utekelezaji
huu ni wa awamu ya kwanza tukimaliza hatua hii tutajenga mtandao wa
mawasiliano chini ya ardhi njia yote inayopita treni na kuhakikisha
mawasiliano yanakuwa mazuri muda wote,tuko katika mazungumzo ya awali na
wadau tutakaoshirikiana nao kutekeelza mradi huu wa kuboresha
mawasiliano kwenye miundo mbinu ya usafri iliyojengwa chini ya
ardhi”.Alisema Delport.
No comments:
Post a Comment