Saturday, July 4, 2015

NEMC WAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI



ut1Mkurugenzi wa  Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota (kulia), akifungua rasmi warsha ya siku mbili ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo  mbalimbali vya habari nchini, kuhusu jinsi ya kuandaa habari za Mazingira, akifungua kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mhandisi Bonaventure Baya, iliyofanyika  katika ukumbi wa Kibo Palace Hotel Mjini Morogoro. Aliyekaa kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano huo  aliyechaguliwa  Bw. Wallace Maugo ambaye pia ni Mhariiri Mtendaji wa gazeti la The Guardian Limited.


ut2
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo  mbalimbali vya habari nchini, wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  Dr. Vedast Makota (hayupo pichani).


ut3
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha.

No comments:

Post a Comment