UNAITAMBUA FANGASI YA MDOMO?,SULUHISHO LIKO HAPA
ziko sababu nyingi zinazoweza
kusababisha hali hii ya kutokea kwenye kinywa, lakini chanzo chake kikubwa ni
maradhi yanayosababishwa na fangasi.
Maradhi ya fangasi ya kinywa huweza
kuathiri koo pia. Vijidudu vinavyoathiri hujulikana kama oral candidiasis na wale wanaoshambulia koo huitwa oesophageal candidiasis.
Utando wa kinywa ni maradhi ni
maradhi yanayosababishwa na vimelea vya fangasi aina ya hamira ambao
hushambulia eneo la ndani ya kinywa na koo.
Kwa kawaida kinga ya mwili pamoja na
vimelea vinavyokaa mwilini vya aina ya bacteria huzuia fangasi hawa
wasiongezeke.
Inapotokea uwiano huu wa kinga ya
mwili na vimelea aina ya bacteria kushindwa kuzuia ongezeko la vimelea hivyo
vya fangasi ndipo hali huwa mbaya na kusababisha utando mdomoni.
Maradhi haya ni kawaida kuonekana
kwa watoto wachanga. Maradhi haya hutokea kutokana na hali ya kutokuwa na
uwiano sahihi kati ya kinga ya mwili wa mtoto na vimelea aina ya bacteria.
Inapotokea yakatokea kwa mtu mzima,
basi mara nyingi huwa kuna viashiria hatarishi kama vile upungufu wa kinga.
Mfano ni watu wenye maradhi ya muda
mrefu kama saratani, kisukari na ukimwi au mwanamke wajawazito, hali hiyo
hushusha kinga zao.
Tatizo hili huwapata pia watu
wanaotumia dawa kwa muda mrefu hususani dawa za vijiuasumu (antibiotic) au za
maradhi yanayotibiwa kwa muda mrefu kama
vile saratani.
Kinachoweza kusababisha hali hiyo
pia ni msongo wa mawazo wa muda mrefu.
Maradhi haya kwa kawaida siyo ya
kuambukiza ingawa mtoto mchanga mwenye maradhi haya huweza kuyaambukiza matiti
ya mama yake.
Dalili ni utando mweupe ambao
huonekana kwenye kinywa eneo la ulimi na mashavuni kwa ndani. Kwenye koo
huonekana kwenye kuta zake.
Mara nyingi eneo lenye rangi nyeupe
huzungukwa na eneo lenye rangi nyekundu na lililovimba kidogo. Hii hutokana na
mashambulizi ya fangasi.
Maeneo haya yaliyoshambuliwa huwa
hayana maumivu makali lakini huweza kutoa damu kama yakiguswa au kusuguliwa.
Dalili nyingine za maradhi ni pamoja
na kuonekana kwa sehemu ndogo zenye rangi nyeupe ndani ya kinywa, kupasuka kwa
midomo, midomo kuongezeka ukubwa, hisia za kukwama kwa chakula kwenye koo,
kuvimba kwa fizi, ladha ya chakula kubadilika na pumzi yenye kutoa harufu.
Kwa watu ambao kinga kinga ya mwili
imeshuka, maradhi haya huweza kusambaa kutoka kwenye kinywa na kushuka kwenye
koo la chakula mpaka kufikia kwenye tumbo.
Hii inapotokea, mgonjwa hupata
maumivu wakati wa kumeza chakula.
Dalili za hatari ni mgonjwa kupata
homa kali ikiambataan na kutetemeka mwili na kushindwa kabisa kumeza chakula.
Mgonjwa akifikishwa hospitali
maradhi haya hutambulika kirahisi kutokana na dalili zake kuweza kutambukiwa
kwa kuangalia kwa macho.
Matibabu ya maradhi haya hutegemea
na kilichosababishwa. Iwapo kilichosababisha kinaweza kuepukwa au kutibika,
basi nayo yataisha, kama mtu ameyapata kutokana na kuugua kisukari, ni vyema
akakitubu kisukari kwanza.
Watoto wachanga hawahitaji matibabu
ya aina yeyote kama dalili zitaanza kuisha kabla ya wiki nne hazijaisha.
On the lips brown
ReplyDelete