Thursday, July 16, 2015

Tanzania yatabiriwa makubwa na wa Italiano.

Kamishna Mkuu wa Maonesho ya Expo Milan 2015, Bruno PasquinoKamishna Mkuu wa Maonesho ya Expo Milan 2015, Bruno Pasquino

WAANDAAJI wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Milan nchini hapa, wameitabiria Tanzania kuwa na uwezekano mkubwa wa kupokea wawekezaji wengi wa vitegauchumi na wafanyabiashara wakubwa, kutokana na kuyatumia maonesho hayo kuzitangaza kikamilifu rasilimali ilizonazo.

Hayo yalisemwa na Kamishna Mkuu wa Maonesho ya Expo Milan 2015, Bruno Pasquino.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania katika maonesho hayo, alisema wawekezaji wengi wanavutiwa na sekta ya utalii na kilimo, ikiwemo cha viungo maeneo ambayo Tanzania imejipanga vizuri kuonesha yaliyomo katika sekta hizo.

“Italia hata kabla ya maonesho haya tumekuwa na mahusiano mazuri katika biashara na uwekezaji, bila shaka hatua yenu ya kushiriki na kujitangaza kikamilifu yatawapa uelewa zaidi washiriki na baadaye kuona maeneo yanayowafaa,” alisema Pasquino.

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika maonesho hayo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad alisema juhudi kubwa zimechukuliwa na Tanzania Bara na Zanzibar, kuweka mazingira mazuri bora kwa wawekezaji vitegauchumi.

Alisema ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo, pia utaipa nafasi kuona kinachofanywa na nchi nyingine.

No comments:

Post a Comment