Tuesday, May 25, 2021

SHAKA AFANYA MAZUNGUMZO NA WASIRA-LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo 25 Mei 2021 ametembelewa na kufanya mazungumzo  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg Steven Masato Wasira katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.


"Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua  hoja kwa mirejesho ya kisiasa, kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi hii"  Mzee Masato  Wasira (MNEC)


"Siku zote  wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa, kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye  hufahamu na kuwa mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawangusha" Shaka Hamdu Shaka. Katibu NEC Itikadi na Uenezi 


MWISHO

No comments:

Post a Comment