Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo 25 Mei 2021 ametembelewa na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg Steven Masato Wasira katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.
"Umefanya kazi
nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu
UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na
kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua hoja kwa mirejesho ya kisiasa,
kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi
hii" Mzee Masato Wasira (MNEC)
"Siku
zote wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa,
kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye hufahamu na kuwa
mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata
walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawangusha" Shaka
Hamdu Shaka. Katibu NEC Itikadi na Uenezi
MWISHO
0 comments:
Post a Comment