Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifatilia kipindi cha maswali na majibu wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Naibu waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu (Mb) wakifatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.
Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo imeyaagiza makampuni ya Premium Agrochem, OCP na Export Trading Group
(ETG) kuhakikisha kwamba ifikapo Julai, 2019 kampuni hizo ziwe na ghala za
kuhifadhia mbolea na mawakala wa kusambaza katika mikoa inayotumia mbolea kwa
wingi ukiwemo mkoa wa Katavi ili kuondoa changamoto ya upungufu wa mbolea kwa
wakulima katika maeneo hayo.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2019
wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe Taska Restituta Mbogo
aliyetaka kufahamu kuwa serikali ina mpango gani wa kusambaza mbolea kwa wakati
katika mkoa wa Katavi.
Alisema
kuwa Serikali inatumia Mfumo wa
Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement
System - BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia
(UREA), Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu
na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.
Mhe Mgumba
aliongerza kuwa Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000
ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia
kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS.
Alisema,
Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa
kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba
2019. Vile vile, ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika
maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa
na tani 147,913 za mbolea.
Aidha, Serikali
inatumia Mfumo
wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement
System - BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia
(UREA). Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu
na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.
Serikali
inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni
mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa
2019/2020 kupitia mfumo wa BPS. Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini
mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo
mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019.
Kadhalika,
Mhe Mgumba alisema kuwa ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa
katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019
kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.
“Serikali
imelielekeza Shirika la Reli Tanzania kutoa kipaumbele cha kusafirisha mbolea
ili kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja na gharama nafuu ili kumfikia
mkulima kwa wakati na bei nafuu” Alikaririwa Mhe Mgumba na kuongeza kuwa
Serikali
inakusanya mahitaji ya mbegu bora na viuatilifu kutoka katika mikoa ili
kuhamashisha kampuni na wafanya biashara kupeleka pembejeo hizo kwa wakulima
kabla ya msimu wa kilimo kuanza na wakati wa mauzo ya mazao.
MWISHO
No comments:
Post a Comment