Wednesday, November 21, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.

Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.

Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.

19 comments:

  1. Fyekelea mbali wanataka kutuletea matatizo hao...Pongezi kwa katibu mkuu na iwe marufuku kwa Africa nzima.

    ReplyDelete
  2. Maamuzi hayo ya serikali nayaunga mkono kwa asilimia 100,yamekuja kwa wakati mwafaka sana hii itasaidia kuondoa na kutokomeza mbinu hatarishi na adui kwa mbegu zetu za asili zinazokuja kwa kigezo cha utafiti wakati lengo lao lipo nyuma ya pazia....GMO!!Genenetic modified???Wanatuletea shida.

    ReplyDelete
  3. Wote tulijua walikuwa wakifanya hayo bila kibali cha serikali. Hongera Sana ndugu katinu mkuu.

    ReplyDelete
  4. Uamzi mzuri kwa.manufaa ya nchi na kizazi kijacho. Hongera sana PS

    ReplyDelete
  5. UAMUZI Huu wa Serikali umenipa amani sana. Hapo sasa tunalinda mbegu zetu za asili

    ReplyDelete
  6. UAMUZI Huu wa Serikali umenipa amani sana. Hapo sasa tunalinda mbegu zetu za asili

    ReplyDelete
  7. Na naipongeza serikali kwa hili na isije ikatolewa kibali kabisa kwa hiyo kitu, tuangalie mbele tupike tukaangamiza vizazi vijavyo....GMO pita kushoto....Hongera sana baba

    ReplyDelete
  8. Big up Hon. Magufuli leadership.We don't want to destroy our own practices

    ReplyDelete
  9. Natamani kujua ni zipi mbegu asili na zisizo asili, na ni mbegu za mimea ipi?

    ReplyDelete
  10. Hatimae Kundi linaloshabikia kupinga GMOs Uhandisijeni Nchini Tanzania kwa mbinu za kuogopesha limeshinda. Je Uamuzi huu utatuweka salama au kutufanya tuwe watazamaji na watumiaji wa bidhaa zenye GMOs usiowrza kuepukika kwa Dunia Kiiiji Sasa! Nakumbuka Mpinzani Mkubwa wa GMOs alivyowahi kukiri siku sio nyingi sana kuwa alikuwa anatumia njia za kudanganya, kutunga na kuogopesha na kusema sio kweli na sasa Tz imeingia mtego huo. PS/KM ashauriwe asiweke total/blanket ban ya Utafiti wa GMO. Upo wa aina nyingi hata Gene Editing na Njia Nyingine Zinazoweza Kutumika kwa Manufaa

    ReplyDelete
  11. Nimependezwa sana na maamuzi haya ya serikali.Huu ni ushindi wa Watanzania wote wa sasa na vizazi vijavyo na pia ushindi dhidi ya uovu.Jina la Bwana libarikiwe sana.

    ReplyDelete
  12. Nimependezwa sana na maamuzi haya ya serikali.Huu ni ushindi wa Watanzania wote wa sasa na vizazi vijavyo na pia ushindi dhidi ya uovu.Jina la Bwana libarikiwe sana.

    ReplyDelete
  13. Kati ya watu 13 waliotoa maoni hadi sasa 11 wanapendezwa na uamuzi wa km. Tujiongeze!

    ReplyDelete
  14. Kati ya watu 13 waliotoa maoni hadi sasa 11 wanapendezwa na uamuzi wa km. Tujiongeze!

    ReplyDelete
  15. Naona Km amefikia hapo kwa ajili ya watafiti husika kutozingatia sheria, kanuni na taratibu yaani "Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali". Watafiti wahusika walipaswa kupeleka matokeo ya tafiti zao serikalini kupitiwa na serikali kujiridhisha kwamba zilizingatia taaluma na tahadhari (precautionary principle) zilizowekwa kisheria. KM yuko sahihi kusitisha hadi hapo serikali imejiridisha kwamba hakuna kasoro za kitaalam na udanganyifu katika takwimu kwa usalama wa watu wetu.

    ReplyDelete
  16. Nadhani tujiongeze, kwa sababu hii field ni pana sana! Kuna mdau ameongea 'Gene editing' na many other benefits. Tusiangalie tu upande mmoja wa shilingi nafikiri tugeuze na upande wa pili,

    ReplyDelete
  17. Naomba tusijeelewa vibaya maamuzi ya KM kama vile ni kukataza utafiti wa GMO nchini, naona amesitisha pilika pilika za watafiti washabiki wa GMO kuanza kutoa matokeo yao bila kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili serikali kujiridhisha. Tafiti na matumizi ya uhandisijeni yapo katika sekta zaidi ya kilimo. Tusisahau mifugo, afya,misitu,samaki, n.k. Hivi karibuni tulisikia habari za mbu waliozalishwa kwa njia ya uhandisi jeni ili kuangamiza malaria, lakini pamoja nia hiyo njema kasoro imejitokeza na kusitishwa mchakato huo kwa utafiti zaidi.

    ReplyDelete
  18. Burning GMO to what extent? Even gene editing from better performing local varieties? No! Am afraid that we will remain stagnant while celebrating certified imported GM products from other countries i.e. apples from SA.
    I think now is the right time to open our eyes and learn from successful and most honoured scientists i.e. Norman Borlaug who contributed to the green revolution e.g. in India due to the food crisis in the 1960's. In that way, Borlaug and his team were able to save many lives from starvation and create reliable food sources.
    Instead of totally burning GM, I think we should focus on establishing/improving our gene banks to preserve potential local varieties within the country and review our regulations and set standards e.g. on "GM to what extent?". All these which requires a detailed research and learning from other successful countries, instead of making a straight forward decision. Ni maoni yangu, asante

    ReplyDelete