METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 2, 2018

WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA BAHARI WILAYANI MTWARA WATAKIWA KULINDA NA KUWAFICHUA WANAODHOOFISHA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

SAM_0928
Pichani ni wawakilishi wa mtandao unaojishughulisha kuratibu utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasirimali za bahari (BMU) kutoka katika halmashauri ya wilaya ya mtwara makoani hapa hivi karibuni wakiwa katika mafunzo maalumu ya siku tano juu ya kuhakikisha rasirimali hiyo inatunzwa ipasavyo ambapo yamefanyikia mjini hapa aliyesimama ni mwezeshaji jamii kutoka mtandao wa usimamizi wa rasirimali za uvuvi shirikishi  nchini (WWF) Geofrey Kamugisha.
SAM_0932
Pichani ni wawakilishi wa mtandao unaojishughulisha kuratibu utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasirimali za bahari (BMU) kutoka katika halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani yapa hivi karibuni wakiwa katika mafunzo maalumu ya siku tano juu ya kuhakikisha rasirimali hiyo inatunzwa ipasavyo ambapo yamefanyikia mjini hapa.
…………………..

Na.Martina Ngulumbi

RAI imetolewa kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa bahari katika halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani hapa kilinda na kuwafichua wale wote wanaodhoofisha juhudi zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo juu ya kuhifadhi rasirimali ya bahari katika halmashauri hiyo.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Omari Kipanga wakati akifunga mafunzo maalumu ya siku tano kwa wawakilishi wa mtandao unaojishughulisha kuratibu utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa rasirimali za bahari (BMU) yaliofanyika mjini hapa huku lengo likiwa ni kuujengea uwezo mtandao huo kuhakikisha malengo yanayokusudiwa yanafikiwa kama inavyotarajiwa.
Amesema, yanapotokea mazingira ya viashiria au vitendo vinavyopolekea kuwepo kwa uharibifu wa bahari ni vema kuwahi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kunusulu kupotea na kuharibu viumbe hai vilivyomo katika rasilimali hiyo ya bahari.
Mwenyekiti wa mtandao huo wa BMU Shaibu Mayonzi kutoka kata ya Msangamkuu amesema kuwa, wakiwa kama wawakilishi wa wananchi katika halmashauri hiyo kwa moyo mmoja wameamua kujitoa kikamilifu kuhakikisha rasirimali hiyo inasimamiwa na kulindwa ipasavyo.
“Siku za nyuma mfano katika eneo langu kulikuwa na matumizi mabaya sana katika hifadhi za bahari kulikuwa na uchafuzi mkubwa wa hahari lakini toka serikali kuwa inatoa elimu ya mara kwa mara hali hiyo imepungua kwa kweli tunaishukuru serikali yetu kwa kutujali”,Amesema Suzana James
Kwa upande wake afisa uvuvi wa halmashauri hiyo Hassan Libwala amesema, tatizo kubwa linalopelekea kuwepo kwa uvuvi huo ni ukosefu wa elimu kwa wavuvi hao na lingine wanafanya kazi kwa mazoea “Mtusaidie ndugu waandishi kutoa elimu kwa wavuvi na wafanyabiashara ya samaki kwani mtu asiingie majini bila leseni na mtu asifanye biashara  bila leseni ni kosa kisheria”,Amesema
Mafunzo hayo yameendeshwa na mtandao wa usimamizi wa rasirimali za uvuvi shirikishi  nchini (WWF) ambapo yameshirikisha kata mbili kutoka katika halmashauri hiyo ikiwemo kata ya Msangamkuu pamoja na Naumbu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com