METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 2, 2018

TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA YA WANAWAKE YAWASILI NCHINI KUCHEZA NA TWIGA STARS

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kutoka Zambia kimewasili mchana huu jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake dhidi ya twiga Stars.
Zambia maarufu kama ‘Shepolopolo’ wametua mchana wa leo Uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa TFF.
Kikosi hicho cha Zambia kitacheza na Twiga Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya mechi hiyo kumalizika, mchezo wa marudiano utafanyika baada ya wiki mbili nchini Zambia.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com