…………………………………………………………………
BENKI ya NMB Tanzania imesema
licha ya kutoa huduma bora kwa wateja wake itaendelea kuhakikisha
inazingatia uwiano wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume ili kuwapa
nafasi wote kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara
ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias katika
mdahalo kuhusu uwaniano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World
Banking ambao unalengo la kuangalia namna bora ya kuwafikia wanawake
katika maeneo mbalimbali duniani ili wapate huduma za kifedha.
Gladness alisema benki hiyo
inatambua umuhimu wa kuwa na uwiano wa kijinsia kuanzia kwa wafanyakazi
wake mpaka aina ya huduma ambazo wanazitoa kwa wateja wake. Alisema NMB
imekuwa na sera bora ambazo zinawapa nafasi sawa wanawake na wanaume
katika vyeo mbalimbali vya ofisi, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo
namna wanaweza kufanya ili kufanikiwa na kwa wajasiliamali kutoa mafunzo
kuhusu njia bora ambayo wanaweza kuitumia kuendeleza biashara zao.
“Uwiano wa kijinsia katika
mashirika ni muhimu ili kuwapa nafasi wanawake washiriki katika shughuli
za maendeleo, kwetu NMB wanawake wanapewa nafasi na hii inatokana na
benki yetu kuwa na sera bora ambazo zinazingatia uwiano uliopo kwa
wafanyakazi wake kuanzia wafanyakazi wetu wa kawaida hadi viongozi
lakini pia tuna Jukwaa la Wanawake ambalo linatumika kutuunganisha
wanawake,”
“Tumekuwa tukitoa mafunzo katika
chuo cha IFM, CBE na UDSM, tunakutana na wanawake na tunawapa historia
zetu jinsi tulivyoweza kufanya na kufanikiwa na wapo ambao wanatamani
kufanya kazi benki tunawapa mbinu ambazo wanaweza tumia kupata nafasi
benki kama unavyojua wanawake wengi wana aibu na hawajiamini hivyo
tunawambia nini wanatakiwa kufanya,” alisema Gladness na kuongeza.
“Jukwaa letu la wanawake
linafanya kazi kwa karibu na kitengo chetu cha Business Bank ambao wao
wanatoa mafunzo kwa Klabu za Biashara (Business Club), wao tumekuwa
tukiwaomba watoe limu kwa wajasiliamali wanawake huko mikoani kama
unavyojua ukiweza kumkomboa mwanakme kiuchumi umekomboa jamii nzima.”
Gladness alisema changamoto kubwa
ambayo inawapata wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na elimu ya namna
wanaweza kutunza taarifa zao za kuuza na kununua bidhaa ili wanapokwenda
benki waweze kupatiwa mikopo kwa urahisi jambo ambalo Business Club
imekuwa ikilitolea mafunzo kwa wajasiriamali.
Aidha Gladness alisema kwa
wajasiriamali wanawake benki ya NMB ina akaunti ambayo inatwa Pamoja
(Pamoja Account) ambayo inatumiwa na vikundi na hivyo kuwataka wanawake
kuitumia akaunti hiyo kwani ina huduma za kisasa ambazo zinaweza
kuwasaida kukuza biashara zao na kuinuka kiuchumi.
“Akaunti ya Pamoja ina huduma
ambazo hazipo katika akaunti za kawaida, wataweza kuona mahesabu yao
vizuri, wanaweza kupata huduma kwenye simu inakuwa sio kama zamani
ambapo ilikuwa ukitaka kuchukua mkopo mpaka mweka hazina awepo lakini
kwasasa wanaweza kutumia NMB Mobile Banking,” alisema Gladness.
0 comments:
Post a Comment