Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akizungumza nao alipotembelea katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ziara ya kikazi katika soko la Ndizi-Mabibo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) akiwasikiliza wananchi wakieleza kero zao wakati wa ziara ya kikazi katika soko la Ndizi-Mabibo. Mwingine ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ubungo Ndg Salum Kali
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika katika Soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dra es salaam
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akizungumza nao alipotembelea katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Julai 14, 2017 amezuia utaratibu uliotaka kutumiwa na Uongozi wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki kilichopo katika Kata ya Mabibo wa kutaka kuwatoa wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dar es salaam kwa madai ya kutaka kujenga Ukuta kwa ajili ya kiwanda hicho.
Mhe Makori alisema kuwa Kauli za tishio la kujengwa ukuta na
kuwaondoa wafanyabiashara wote katika soko hilo alizipata jana mchana
(13/7/2017) na kuamua kufanya mkutano na wananchi sambamba na wafanyabiasha katika
soko hilo.
Mkuu wa Wilaya ya ubungo Mhe Makori amemuagiza Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo ndg john lipesi Kayombo kutotoa kibali cha ujenzi wa ukuta
unaotaka kujengwa na Uongozi wa Kiwanda cha nguo cha Urafiki mpaka pale
watakapofuata utaratibu.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeagiza
kuwaondoa wafanyabiashara hususani machinga endapo tu kama kuna maeneo ya
kuwapeleka katika maeneo rafiki watakapofanya biashara kwa Amani pasina
mashaka.
“Kwa kuwa wafanyabiashara hawa bado hatujaainisha eneo la kuwapeleka
kwahiyo nakuagiza leo Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha hawaondoki kwani
wanalipa kodi kwa ufasaha hivyo sihitaji wasumbuliwe na mtu yoyote”
“Kama wafanyabiashara hawakwepi kodi kwanini kikundi kimoja
cha wala rushwa ndicho kianze kutaka kuwagombanisha wananchi na kuichukia
serikali yao kisa tu tumeziba mianya yao ya ulaji ” Alisema Mhe Makori
Mhe Makori alisema kuwa kuna kikundi cha wafanyabiashara katika
soko hilo kinaitwa Majimoto ndicho ambacho kinachochea kadhia hiyo ya
kuhamasisha uongozi wa kiwanda hicho kuanza chokochoko za kutaka kuwafukuza
wafanyabiashara hao.
Sambamba na hayo pia Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kuwaagiza wataalamu wa Mazingira ili kufatilia kiwanda hicho ambacho kinalalamikiwa na wananchi kuathiri afya zao kutokana na Moshi unaotoka kiwandani hapo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO
0 comments:
Post a Comment